Kwa Mujibu wa Shirika la habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Mandela, Mjukuu wa Nelson Mandela, Mpiganaji mkubwa wa Kiafrika na Kiongozi wa Upinzani (Muqawamah) wa ndani dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa nchi hii kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa kidemokrasia, alisema wakati wa uwepo wake katika Marasimu (Hafla) ya Mazishi ya Miili ya Mashahidi wa Umma wa Kiislamu, Sayyida Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyud-din huko Beirut kwamba hao (Wazayuni) Walimuua (Sayyid Hassan Nasrullah); Lakini mawazo yake yataendelea kuwepo miongoni mwa wapigania uhuru wote duniani, kwani Afrika Kusini tunasema hajafa bali amezidishwa mara dufu.
Mnamo tarehe 23 Februari, idadi kubwa ya watu huru kutoka duniani kote walikuja Beirut kushiriki katika mazishi ya Mashahidi wa Umma wa Kiislamu, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiyyud-din, ambao ni katika kizazi cha Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah hakuwa Katibu Mkuu pekee wa Hezbollah; Bali alikuwa ni Katibu Mkuu na Kiongozi wa Waarabu, Waajemi, Wazungu, Weusi na wanyonge wote Duniani. Alikuwa Kiongozi wa kihistoria katika kukabiliana na ubeberu na nguvu za uistikbari na kiburi cha Kimataifa, na akawa alama na mfano kwa kila mpiganaji katika sayari hii.
Shahidi Nasrallah anasalia kuwa mfano wa kuigwa kwa wapiganaji na wapenda uhuru wote duniani
Mwanzoni mwa mazungumzo haya, Mandela alisema kuhusu maana ya ushiriki wake kutoka Afrika Kusini katika hafla ya maziko ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiyyud-din: Tumetembelea mahali alipouawa Shahidi Kiongozi wetu Mkuu, Sayyid Hassan Nasrallah.
Wao (Wazayuni) walimuua kishahidi, lakini mawazo na fikra zake zitabaki kwenye nyoyo na akili za kila mpigania uhuru duniani kote. Tunasema huko Afrika Kusini, hajafa, lakini amezidishwa mara dufu. Tunaheshimu kumbukumbu ya shujaa huyu na ushujaa wake na tunashukuru uongozi na wanachama wa Hezbollah kwa utetezi wao wa kijasiri wa Msikiti wa Al-Aqsa, watu wa Gaza na Muqawamah wote wa Palestina.
Shakhsia huyu mashuhuri wa Afrika Kusini alisema kuhusu umuhimu wa kauli mbiu isemayo "Sisi tunabakia katika ahadi yetu" katika mapambano dhidi ya ubeberu na nguvu za kiburi na uistikbari wa kimataifa, na vile vile kuunga mkono Palestina: Kwa kauli mbiu hii, tunatangaza uungaji mkono wetu kamili kwa wale wote wanaopigania ukombozi wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (na utawala haramu wa kizayuni), wakiwemo makundi ya Muqawamah ya Palestina, yanayoongozwa na Hamas na harakati ya Jihad ya Kiislamu, Hezbollah ya Lebanon, Ansarullah ya Yemen, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na wale wote wanaounga mkono mapambano ya Palestina katika eneo hilila kikanda.
Amesema: Tunamuomba kila mtu Kusini mwa Dunia kuambatana na msimamo wa kijasiri wa kuunga mkono Muqawamah wa Palestina. Wote hao wanapaswa kufuata mfano wa ushujaa wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah ambaye alibaki imara kwenye njia hii bila ya woga wowote na kuamini ushindi dhidi ya ubeberu wa Magharibi na akauona kuwa ni wa uhakika.
Mandela alisema kuhusu tathmini yake juu ya mahudhurio makubwa ya watu kutoka mabara mbalimbali ya dunia katika hafla ya mazishi ya Masayyid wa Mashahidi, na Mashahidi wa Umma wa Kiislamu, na jinsi shule ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah ilivyoweza kuziteka nyoyo za watu na mabara yote: Tunawashukuru mamilioni ya wapenda uhuru duniani kote wanaoshiriki usiku na mchana katika mikusanyiko na maandamano, kususia kampeni dhidi ya utawala wa Kizayuni, na maandamano ya kuwaunga mkono Wananchi wa Palestina, na tunawaambia kwamba sauti yenu inasikika huko Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Beirut, na kwamba ushindi unakaribia kwa Mapenzi na matakwa ya Mwenyezi Mungu.
Mwishoni, Mjukuu wa Nelson Mandela alitoa salamu na kuthamini misimamo shupavu ya Taifa na Uongozi wa Yemen, ambao licha ya hali yao ngumu katika kivuli cha vita na mzingiro uliowekwa na adui, wanaendelea kuchukua hatua za kupinga ubeberu.
Your Comment